Yanga SC

YANGA: BADO TUNAO UWEZO WA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

admin May 16, 2021 10:47 am


NAHODHA msaidizi wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ambaye ni beki wa kati amesema kuwa bado timu hiyo inayo nafasi ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Jana Mei 15 ubao wa Majaliwa baada ya dakika 90 ulisoma Namungo 0-0 Yanga na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Sare hiyo inawafanya Yanga wafikishe jumla ya pointi 58 baada ya kucheza mechi 28 huku Namungo FC ikiwa nafasi ya 10 na pointi zake ni 36 baada ya kucheza jumla ya mechi 26.

Mwamnyeto amesema:-“Mechi ilikuwa ngumu lakini tunashukuru Mwenyezi Mungu tumetoka sare.

“Bado tunao uwezo wa kuchukua ubingwa, tumetoka sare hatujapoteza, tunaweza kupata pointi tatu za JKT Tanzania tukakaa vizuri,”. 

Kwa sasa bingwa mtetezi ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ikiwa imekusanya pointi 61 baada ya kucheza mechi 25.

GOMES: BADO TUNA MATUMAINI YA KUPATA MATOKEO COASTAL UNION YAPOTEZA POINTI TATU MBELE YA POLISI TANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply