Yanga SC

YANGA AKILI ZAO ZOTE NI KWENYE MECHI ZAO ZIJAZO

admin May 17, 2021 8:47 pm


 BAADA ya kumalizana na Namungo FC kwenye sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa kwa sasa hesabu za Yanga ni mbele ya JKT Tanzania.

Mchezo wao dhidi ya Namungo ilikuwa ni Mei 15 na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Namungo 0-0 Yanga jambo lililowafanya wagawane pointi mojamoja.

Kituo chao kinachofuata ni dhidi ya JKT Tanzania, Mei 19 Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa ngoma ilikamilika Yanga 1-0 JKT Tanzania hivyo utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa.

Nahodha msaidizi wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zilizobaki ili kufikia malengo waliyojiwekea.

“Bado tuna kazi ya kufanya na kwa sasa akili zetu ni kwenye mechi ambazo zinafuata na imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri,” .

UTATA WA BAO LA YANGA MBELE YA NAMUNGO FC UMEMALIZWA NAMNA HII MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply