Home Simba SC SIMBA HESABU ZAO NI KUPINDUA MEZA KWA MKAPA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA HESABU ZAO NI KUPINDUA MEZA KWA MKAPA LIGI YA MABINGWA AFRIKA


 WAKATI wadau wengi wa soka wakiamini kuwa ndoto za Simba kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika zimeyayuka kufuatia kichapo cha mabao 4-0, lakini hali hiyo ni tofauti kwa Kocha Didier Gomes ambaye anaamini kuna maajabu yatatokea kwa Mkapa.

 

Gomes alisema raha ya mpira ni sayansi iliyopo wazi, kwani kama kuna watu waliamini watashinda ugenini au kutoka sare na mwishowe wakafungwa, basi hata kwa Mkapa kuna matokeo yasiyotarajiwa na wengi yanaweza kutokea.

 

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa wa Afrika Kusini, Soccer City, Gomes alisema licha ya kupoteza kwa mabao mengi haina maana kuwa walicheza vibaya.


“Tulifungwa siyo kwa sababu hatukucheza vizuri, tulikuwa bora uwanjani na tulifanya kila kitu tulichopanga ila bahati haikuwa kwetu na ile ndiyo tafsiri ya soka, hakuna ambaye anaweza kulitabiri.

 

Hatujatolewa kwenye mashindano kwa sababu bado tuna dakika 90 zingine tukiwa Dar es Salaam, naamini kuna jambo tunaweza kufanya, kwa sababu mpira ni sayansi ambayo ipo wazi,” alisema Gomes.


Baada ya kupoteza mchezo huo wakiwa nyumbani, Simba wanajipanga kwa mchezo wa marudio utakaopigwa Mei 22 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na wanatakiwa kushinda mabao 5-0 ili waweze kutinga hatua ya nusu fainali.

 

SOMA NA HII  MCHEZO WA SIMBA V POLISI TANZANIA WAPELEKWA MBELE