Yanga SC

YANGA YAWAFUATA JKT TANZANIA DODOMA

admin May 18, 2021 4:47 am


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Nassreddine Nabi leo Mei 18 kimeanza safari kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania. 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Mei 19, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma majira ya saa 10:00 jioni.

Baadhi ya wachezaji ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Feisal Salum, Bakari Mwamnyeto, Ramadhan Kabwili, Zawad Mauya na Metacha Mnata.

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, Yanga ilisepa na pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0.

Hivyo mchezo ujao utakuwa na ushindani kwa timu zote mbili ambapo JKT Tanzania watahitaji kulipa kisasi na Yanga wao watahitaji kulinda rekodi zao.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili na pointi zake kibindoni ni 58 inawafuata JKT Tanzania walio nafasi ya 13 na pointi 33.


MAGUIRE HATIHATI KUIKOSA FAINALI YA EUROPA MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA KWA SASA UPO NAMNA HII UTAZAME

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply