Ligi Kuu

HIZI HAPA LEO KUSAKA USHINDI NDANI YA LIGI KUU BARA

admin May 19, 2021 12:47 pm


 LEO Mei 19 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo kuna mechi mbili zinachezwa ili kusaka pointi tatu muhimu.

Mchezo wa mapema kabisa ni ule utakaowakutanisha Gwambina FC dhidi ya Namungo ambao unapigwa Uwanja wa Gwambina Complex.

Tayari Gwambina wameanza kusaka pointi tatu kama ilivyo Namungo, ambapo mchezo huo umeanza majira ya saa 8:00, Mwanza.

Pia mchezo huo wa Gwambina FC dhidi ya Namungo upo mubashara Azam TV ukikamilika huo unafuata ule wa JKT Tanzania dhidi ya Yanga.

Mchezo huo utachezwa saa 10:00 jioni na ni Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA JKT TANZANIA VPL: JKT TANZANIA 0-2 YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply