CAF

NYOTA WAWILI WA KAIZER CHIEFS KUIKOSA SIMBA KWA MKAPA

admin May 19, 2021 6:47 am


 NYOTA wawili wa kikosi cha Kaizer Chiefs wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ni wa robo fainali ya pili unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22. 

Wachezaji hao ni pamoja na kiungo Khama Billiant raia wa Zimbabwe na Dumisani Zuma ambao wanasumbuliwa na majeruhi.

Simba ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 baada ya ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa FNB Soccer Citym ubao kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba.

Uongozi wa Simba uliweka wazi kwamba una mlima mzito wa kusaka ushindi kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

Kikosi cha Kaizer Chiefs kinatarajiwa kutua ndani ya wiki hii ili kufanya maandalizi ya mwisho huku tayari wakiwa wameshatumwa wawakilishi wao Bongo kuandaa mazingira. 

GUARDIOLA KUFAYA MAAMUZI MAGUMU JUU YA AGUERO JKT TANZANIA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply