DOZI ambayo inatolewa kwa sasa na Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, raia wa Ufaransa kwa wachezaji wake ni hatari kwa kuwa ni bandika bandua, bila kuonyesha tabasamu kwa wachezaji hao.
Picha ipo hivi mara baada ya ubao wa Uwanja wa FNB City Soccer City kusoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba, siku ya pili walianza mazoezi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Mei 22, Uwanja wa Mkapa.
Kikosi kiliporejea Bongo, Mei 17, wachezaji walipumzika kwa masaa kadhaa kabla ya jana asubuhi kurejea mazoezini kisha mchana kupiga tizi lingine na jioni tena dozi kuendelea.
Hivyo kwa siku wanafanya mazoezi mara tatu ili kuweza kulipa kisasi mechi yao ijayo kwa kuwa malengo yao ni kutinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taarifa kutoka benchi la ufundi zimeliambia Championi Jumatano kuwa:”Hakuna kupumzika kwa sasa ni kazi muda wote, asubuhi, mchana na jioni ni dozi, hakuna muda wa kucheka tena, kazi inaendelea,”.
Habari zinaeleza kuwa program ya asubuhi, mchana na jioni kila program inatumia masaa matatu hivyo wachezaji wanatumia muda wa masaa tisa kuivutia kasi Kaizer Chiefs bila kucheka.
Meneja wa Simba, Patrcik Rweyemamu ameliambia Championi Jumatano kuwa wanajiandaa vema ili kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao ujao.