WEKA mbali kuyeyuka kwa ndoto ya wawakilishi wa Tanzania, Simba katika hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutinga hatua ya nusu fainali, kuna rekodi ya nyota wao Clatous Chama ameiweka katika mashindano hayo ya kimataifa.
Nyota huyo ambaye amekuwa bora ndani ya Simba anashikilia rekodi ya kuwa mtaalamu wa kufunga mabao ya dakika za usiku pale anapopata nafasi ya kufunga Uwanja wa Mkapa.
Ukiacha mbali rekodi yake ya Mei 22, Uwanja wa Mkapa uliposoma Simba 3-1 Kaizer Chiefs wakati Chama alipopachika bao dakika ya 86 kwa pasi ya mshikaji wake Luis Miquissone ana mabao mengine aliyapachika nyuma dakika za usiku kwenye ligi za mabingwa Afrika namna hii:-
Machi 16, 2019, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-1 AS Vita ilikuwa ni hatua ya makundi, Chama alipachika bao dakika ya 89.
Desemba 23,2018 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 3-1 Nkana,Chama alipachika bao la mwisho na la ushindi dakika ya 90.
Novemba 28,2018, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 4-1 Mbabane Swallows, Chama alipachika bao la usiku dakika ya 90+1 ilikuwa ni hatua ya awali.