Simba SC

SIMBA YASEPA NA POINTI TATU MAZIMA ZA NAMUNGO, MAJALIWA

admin May 29, 2021 3:47 pm


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo Mei 29 kimesepa na pointi tatu mazima mbele ya Namungo FC.

Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Namungo 1-3 Simba.

Ni Styve Nsigimasabo alianza kumtungua Aishi Manula dakika ya 21 na kuwafanya Namungo kuutawala mchezo dakika 45 za mwanzo.

Kipindi cha pili Simba ilianza kurudi kambani kwa kupitia Chris Mugalu dakika ya 78, nahodha John Bocco dakika ya 83.

Msumari wa mwisho ulipachikwa na mzee wa kukera Bernard Morrison ambaye alipachika bao hilo akiwa nje ya 18 kwa shuti lililomshinda mlinda mlango, Nahimana Jonathan.

Simba inafikisha pointi 64 ikiwa nafasi ya kwanza Namungo nafasi ya 8 na pointi 40.

TANZIA: CLATOUS CHAMA AFIWA NA MKE WAKE NCHINI ZAMBIA SHERIA YA BAO LA UGENINI LAFUTWA UEFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply