Home Yanga SC ALICHOSEMA MUKOKO KUHUSU DILI LA KUJIUNGA NA HOROYA YA GUINEA

ALICHOSEMA MUKOKO KUHUSU DILI LA KUJIUNGA NA HOROYA YA GUINEA

KIUNGO wa Yanga, Tonombe Mukoko anahusishwa kuhitajika na klabu ya Horoya inayoshiriki Ligi Kuu nchini Guinea baada ya kuonyesha kiwango kizuri msimu huu.

Mukoko alijiunga na Yanga akitokea AS Vita ya DR Congo msimu huu akisaini mkataba wa miaka miwili na amekuwa na msaada mkubwa eneo la kiungo.

Akizungumza na SokalaBongo,kiungo huyo alisema yupo tayari kwenda kucheza soka nchini humo lakini kwa sasa anawaachia mabosi wake Yanga kuamua hilo kama watafikia makubaliano ya kimasilahi kwa pande zote mbili.

“Mimi ni mchezaji na ninafurahi kuwa hapa, Yanga ni timu kubwa Afrika kama zilivyo timu nyingine lakini kama kuna timu inanihitaji basi wakielewana na Yanga naweza kuondoka.”

Inaelezwa Horoya wamepeleka ofa ya Dola 200,000 (Sh463 milioni) kwa klabu na mshahara wa Dola 9000 (Sh20 milioni) kwa mwezi upande wa mchezaji.

Kama Yanga wataamua kumwachia mchezaji huyo basi itakuwa ni mara ya pili kwa klabu hiyo kufanya biashara na timu hiyo baada ya awali kumuuza mshambuliaji Herieter Makambo.

Dili hilo kama litakamilika basi Yanga watalazimika kuingia sokoni kusaka mrithi wa Mukoko.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTUPIA GOLI 2 JUZI....GAMONDI KAIBUKA NA HILI KUHUSU GUEDE NA UWEZO WAKE...