Home Yanga SC HII HAPA ORODHA YA MAJEMBE YA KAZI YA NABI NDANI YA YANGA

HII HAPA ORODHA YA MAJEMBE YA KAZI YA NABI NDANI YA YANGA


 NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga,  tayari amekata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ambalo lipo mikononi mwa watani zao wa jadi Simba.

Hatua hiyo ameifikia baada ya ubao wa Kambarage, jana Mei 25 kusoma Mwadui 0-2 Yanga huku tayari akiwa ameshapata majembe yake ya kazi baada ya kurithi mikoba ya Cedric Kaze.

  Tayari ameshapata majembe yake manne ya kazi kwa upande wa ulinzi ambayo amekuwa akiyatumia mara kwa mara.

 

Nabi raia wa Tunisia, amekiongoza kikosi hicho katika mechi tano ambapo alishinda tatu, sare moja na kupoteza moja ndani ya dakika 450.

 

Kwa upande wa safu ya ulinzi anamuamini Metacha Mnata ambaye rekodi zinaonesha kwamba alikaa langoni kwenye mechi tatu, alikosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC pamoja na wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mwadui FC, Kibwana Shomary na Adeyum Saleh, wote wamecheza mechi zote tano.

 

Kwa upande wa Dickosn Job, amecheza mechi nne na hakuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Prisons wa Kombe la Shirikisho.


Mbali na nyota hao wanne ambao ni chaguo lake la kwanza, pia yupo Bakari Mwamnyeto ambaye ameanza kikosi cha kwanza mechi tatu na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambao kwenye mechi tano alianza kikosi cha kwanza katika mechi mbili, ikumbukwe kwamba Shaibu alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, JKT Tanzania na Mwadui FC kwa kuwa ni mejeruhi.

 

Nahodha Lamine Moro alianza kikosi cha kwanza mchezo mmoja, ulikuwa wa Kombe la Shirikisho mbele ya Tanzania Prisons, ila kwa sasa amepigwa pini kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu.

 

Mechi zake Nabi ndani ya Yanga  ilikuwa ni Aprili 25 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 0-1 Azam FC.

 

Kombe la Shirikisho, Aprili 30 hatua ya 16, Tanzania Prisons 0-1 Yanga. Mei 15, Namungo 0-0 Yanga na Mei 19, JKT Tanzania 0-2 Yanga. Mei 25, Mwadui 0-2 Yanga ilikuwa ni hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  ISHU YA MWINYI ZAHERA KUWA MKALIMALI YANGA IPO HIVI


Nabi aliliambia Spoti Xtra kuwa, kila mchezaji ana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kutokana na juhudi ambazo atazionesha katika mazoezi.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here