Home Yanga SC JKT TANZANIA YAYEYUSHA POINTI TATU MAZIMA MBELE YA YANGA

JKT TANZANIA YAYEYUSHA POINTI TATU MAZIMA MBELE YA YANGA


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi leo Mei 19 kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ni Yacouba Songne alipachika bao la kwanza dakika ya 27 bao la pili lilifungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 30.

Hivyo leo Yanga imeondoka Uwanja wa Jamhuri kifua mbele huku JKT Tanzania ikiyeyusha pointi tatu mazima ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29 baada ya kucheza mechi 29 na JKT Tanzania nafasi ya 14 baada ya kucheza mechi 30.

SOMA NA HII  NABI:- YANGA HATUTARUDIA MAKOSA KWA MAZEMBE...