Home Yanga SC MASHINE ZA KAZI ZA YANGA ZINAZOIVUTIA KASI MWADUI FC HIZI HAPA

MASHINE ZA KAZI ZA YANGA ZINAZOIVUTIA KASI MWADUI FC HIZI HAPA


 KIKOSI cha Yanga kwa sasa kinaendelea na maandalizi ya mwisho ya mchezo wake wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa kesho, Mei 25.

Itakuwa ni dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na mshindi wa mchezo huo anatarajiwa kukutana na Biashara United ya Mara ambayo ilishinda jana kwa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanaendelea na mazoezi ni pamoja na mshambuliaji wao mwili jumba, Michael Sarpong ambaye alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania.

Pia Farid Mussa ambaye ni kiungo huyu alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kutibu majeraha yake ila kwa sasa tayari amesharejea .

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa Farid Mussa yupo imara na ataendelea kuwapa burudani Wananchi.

Nyota wengine ni pamoja na Bakari Mwamnyeto, Metacha Mnata, Dickson Job, Kibwana Shomari, Adeyum Saleh, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Wazir Jr, Feisal Salum, Yacouba Songne, Faroukh Shikalo, Raadhan Kabwili, Saido Ntibanzokiza.

Nyota hao wote wapo chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi, raia wa Tunisia ambaye anakumbukumbu ya kutoka kukiongoza kikosi hicho kushinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa ligi.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA AZAM.....MANARA KAONA ISIWE TABU...LEO KAIBUKA NA HILI JIPYA...