Home CAF MTAFUTANO WA SIMBA DHIDI YA KAIZER CHIEFS BALAA

MTAFUTANO WA SIMBA DHIDI YA KAIZER CHIEFS BALAA


KAZI bado inaendelea ambapo kwa sasa kikosi cha Simba kinaendelea kuwavutia kasi wapinzani wao Kaizer Chiefs.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho, Mei 22, Uwanja wa Mkapa huku Simba wakitakiwa kushinda jumla ya mabao 5-0 ili kusonga mbele kwa kuwa mchezo wa kwanza walikubali kichapo cha mabao 4-0 jambo ambalo waliweka wazi kwamba ni mlima mzito.

 Mtafutano wa ushindi mbele ya Kaizer Chiefs kwa kikosi cha Simba umezidi kuwa mkali ambapo Kocha Mkuu, Didier Gomes ameamua kuja na mbinu mpya ya kushambulia kwa kushtukiza na kujilinda kwa umakini.

Ni katika mazoezi ambayo yanaendelea kwa kikosi hicho kwenye Viwanja vya Mo Simba Arena ambapo kazi inaendelea kwa wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.

Jana Mei 20 iliendelea na mazoezi ambapo yaligawanywa mafungu mawili kwa wachezaji hao ili kutengeneza kasi pamoja na mbinu kwa kila mmoja.

Gomes aligawa la kwanza ambalo lilikuwa namna hii:-Luis Miquissone, Mzamiru Yassin, Pascal Wawa, John Bocco, Rally Bwalya, Clatous Chama, Mohamed Hussein, Chris Mugalu, Joash Onyango na Shomari Kapombe na Aishi Manula.

Kazi ilikuwa moja kwa wachezaji hawa kupambana kusaka ushindi kwa washkaji zao ambao walikuwa ni kundi la pili nalo lilikuwa namna hii:-

Meddie Kagere, Ibrahim Ame, Bernard Morrison, Gadiel Michael, David Kameta, Said Ndemla, Ibrahim Ajibu, Miraji Athuman, Perfect Chikwende, Francis Kahata, Hassan Dilunga na Beno Kakolanya.

SOMA NA HII  CHAMA,MUSONDA WAREJEA ZAMBIA..... ISHU IKO HIVI