Home Simba SC NYOTA HUYU WA MABAO AINGIA ANGA ZA SIMBA

NYOTA HUYU WA MABAO AINGIA ANGA ZA SIMBA


 IMEELEZWA kuwa mtambo wa kutengeneza mabao ndani ya Kagera Sugar, David Luhende yupo kwenye hesabu za kutua Simba msimu ujao.

Habari zimeeleza kuwa nyota huyo amekuwa kwenye uangalizi mkubwa na watu wa Simba ambao wanahitaji kumnasa pale msimu utakapomeguka 2020/21.

Ndani ya Kagera Sugar, Luhende ameweka rekodi ya kucheza jumla ya mechi 30 na ametoa pasi 7 za mabao akitupia mabao mawili yote kwa mapigo huru.

Aliwatungua Azam FC akiwa nje ya 18 na aliwatungua pia Mwadui FC nje ya 18 ikiwa ni mapigo huru.

“Luhende yupo kwenye hesabu za kutua Simba hivyo kwa wachezaji wazawa chaguo namba moja ni yeye ikiwa kutakuwa na mabadiliko itakuwa kidogo sana,” ilieleza taarifa hiyo.

SOMA NA HII  BOCCO ASEPA NA TUZO YA MCHEZAJI BORA