Home Azam FC TUMBO LILIMVURUGA PRINCE DUBE MBELE YA RHINO RANGERS

TUMBO LILIMVURUGA PRINCE DUBE MBELE YA RHINO RANGERS

 VIVIER Bahati,  Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa mshambuliaji wao namba moja Prince Dube yupo vizuri licha ya jana kutomaliza dakika 90 mbele ya Rhino Rangers. 

Wakati ubao wa Kambarage,  Shinyanga ukisoma Rhino Rangers 1-3 Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho,  hatua ya robo fainali, Dube alitumia dakika 8 katika mchezo huo.

Walitolewa nje chini ya uangalizi wa madaktari wa Azam FC baada ya kushindwa kuendelea kucheza kwa kile kilichoelezwa kuwa ameumia.

Bahati amesema:”Dube yupo vizuri,  kabla ya mchezo alikuwa anasumbuliwa na tumbo ila lilikuwa sawa akaanza kucheza na alipoanza kucheza,  tumbo likamsumbua tena hivyo alitolewa na kupewa huduma ila kwa sasa yupo vizuri, “.

Ndani ya Ligi Kuu Bara ni namba moja kwa kutupia akiwa na mabao 14 akifuatiwa na Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 11.

Mchezo wao wa nusu fainali itakuwa dhidi ya Simba iliyoshinda mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji, utakaochezwa Uwanja wa Majimaji, Songea.

SOMA NA HII  AZAM FC WAJIBU MAPIGO SIMBA....NAO WASHUSHA KIFAA CHA MAANA KUTOKA GHANA...HUYO OKRAH CHA MTOTO...