Home Yanga SC YANGA WABAINISHA SABABU YA NYOTA WAKE YASSIN NA CARLINHOS KUACHWA

YANGA WABAINISHA SABABU YA NYOTA WAKE YASSIN NA CARLINHOS KUACHWA


 UONGOZI wa Klabu ya Yanga umefunguka kuwa sababu kubwa ya nyota wao wawili, Carlos Carlinhos na Yassin Mustapha kuendelea kukosekana kwenye kikosi hicho ni kutokana na nyota hao kupata majeraha ya kuchanika misuli ya paja.

 

Yassin alipata majeraha hayo akiwa na kikosi cha Taifa Stars na hajaonekana uwanjani tangu Aprili 10, mwaka huu ambapo mpaka sasa amekosa michezo minne ya Yanga, dhidi ya KMC, Biashara Unied, Gwambina na Azam FC.

 

Carlinhos yeye alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Nyota hao wote wameachwa na kikosi cha Yanga kilichoenda mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC utakaopigwa leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kuhusiana na Yassin Mustapha yeye alichanika msuli wa nyama ya paja akiwa na kikosi cha taifa, alivyorejea kujiunga na wenzake klabuni alikuwa akihisi maumivu.

 

“Tulipomfanyia vipimo akagundulika alipata hilo tatizo, na akapewa wiki mbili za mapumziko ambayo yanatarajia kumalizika wiki ijayo.

 

“Kuhusiana na Carlinhos naye alichanika msuli katika mchezo wetu dhidi ya Namungo kutokana na kuutanua msuli kuliko inavyotakiwa ‘over stretch’, ambapo naye alipewa wiki mbili za mapumziko pamoja na matibabu ili kupona kabisa.”

SOMA NA HII  GUEDE APEWA MECHI MBILI TU YANGA....AKIZINGUA 'ANAPIGWA CHINI CHAP' HARAKA...