Home Uncategorized ALLIANCE WAIVURUGA MWADUI FC, WALIPA KISASI CHA AZAM FC

ALLIANCE WAIVURUGA MWADUI FC, WALIPA KISASI CHA AZAM FC


DAVID Richard mshambuliaji wa Alliance jana alisepa na mpira wake mbele ya Mwadui FC Uwanja wa Nyamagana kwnye ushindi wa mabao 4-1 na kulipa kisasi cha Obrey Chirwa aliyeifunga timu hiyo mabao matatu.

Richard anakuwa mshambuliaji wa tano kusepa jumla na mpira kwenye ligi msimu wa 2019/20.

Mshambuliaji wa kwanza kusepa na mpira alikuwa ni Ditram Nchimbi mbele ya Yanga wakati akiwa Polisi Tanzania, Daruesh Saliboko wa Lipuli mbele ya Singida United.

Obrey Chirwa mbele ya Alliance na Kelvin Sabato mbele Mwadui.

Ushindi huo unaifanya Alliance kuwa nafasi ya 13 na pointi 23 huku Mwadui FC ikiwa nafasi ya 19 na pointi 19.

SOMA NA HII  MECHI 100 ZA SALAH ZINA MSOTO WA KUTOSHA BALAA