news

RUVU SHOOTING YAPOTEZA MBELE YA SIMBA, UBAO UMESOMA 0-3

admin June 3, 2021 3:50 pm


KIKOSI cha Simba leo Juni 3, kimeshuhudia ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba,  ukisoma Ruvu Shooting 0-3 Simba.


Ni katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu muhimu.


Ni John Bocco ambaye ni nahodha wa Simba alitupia bao la Kwanza dakika ya 17 na lile la pili dakika ya 87.


Bao la tatu ni mali ya Chris Mugalu dakika ya 61 ambaye aliwafanya mashabiki wa Simba kuongeza shangwe na kusepa na pointi tatu mazima. 


Ule wa Kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru ubao ulisoma Simba 0-1 Ruvu Shooting hivyo leo Simba wamelipa kisasi.

LYANGA AJIPIGA PINI AZAM FC MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply