news

THOBIAS KIFARU: TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO CHANYA

admin June 4, 2021 9:48 am


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba kwa sasa mipango yao ni kupambana kupata matokeo chanya kwenye mechi zao ambazo zimebaki.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa tayari wameanza maandalizi kwa ajili ya mechi zao zilizobaki na wanaamini watafanya vizuri.

“Mtibwa Sugar kweli kwa sasa tumeamua kuona namna gani tutakuwa bora hasa kwa mechi zetu ambazo zimebaki na tunaamini kwamba tutafanya vizuri kupata matokeo chanya.

“Kikubwa ni kwamba kuanzia wachezaji mpaka benchi la ufundi linajua kwamba hatupo sehemu salama kwa sasa ila kila kitu kitakuwa sawa kwani tayari maandalizi yameanza na tuna imani ya kubaki ndani ya ligi,” amesema.

Kwenye msimamo Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 na pointi 34 baada ya kucheza jumla ya mechi 30. 

DAKIKA YA 80, MOLINGA BADO ANAONGOZA KWA WASHAMBULIZI YANGA YANGA: MECHI YETU DHIDI YA SIMBA UKITUAMSHA USIKU TUNACHEZA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply