Yanga SC

YANGA: MECHI YETU DHIDI YA SIMBA UKITUAMSHA USIKU TUNACHEZA

admin June 4, 2021 9:48 am


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba hauhitaji maandalizi kwenye mchezo wao ambao utawahusu watani wao wa jadi Simba hata wakiamshwa usiku wataingia uwanjani kucheza bila mashaka.

Mchezo wao wa awali ambao ulipaswa kuchezwa Uwanja wa Mkapa uliyeyuka baada ya watani hao wa jadi kueleza kuwa wanafuata kanuni kutokana na Bodi ya Ligi Tanzania kubadili muda ghafla ikiwa ni masaa machache kabla ya mchezo huo. 

Kufuatia kuahirishwa kwa mchezo huo Bodi ya Ligi ilipanga mchezo mwingine kuchezwa Julai 3 na Yanga kupitia kwa Ofisa Habari, Hassan Bumbuli aliweka wazi kwamba wana mechi nne ambazo zimebaki na hizo watawekeza nguvu kubwa kwa maandalizi.

Bumbuli amesema:”Mchezo wetu sisi dhidi ya Simba hauhitaji maandalizi hata tukiamshwa usiku sisi tunacheza na hata tukiamka asubuhi sisi tunacheza hatuna tatizo nao.

“Nilisema kwamba tumebakiwa na mechi nne ambazo ni fresh kwa sababu hizo zipo kwenye ratiba na hata mwalimu anajua kwamba hizo zipo na tutafanya vizuri.

“Kuhusu mechi ya Simba, Julai 3 hiyo ipo kama ambavyo imepangwa na Yanga haijatoa tamko kuhusu mechi hiyo hivyo kilichopo ni kuona kwamba tunajiandaa. Ule ni mchezo wa kiporo hauna mambo mengi tupo tayari,” amesema. 

THOBIAS KIFARU: TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO CHANYA VIDEO: MASHABIKI WA SIMBA WATUMA SALAMU KWA YANGA, WADAI WANAOGOPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply