UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa kikosi kimerejea kambini kwa ajili ya mechi zao za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa mipango inakwenda sawa na wanaamini kwamba kila kitu kitakuwa sawa.
Bumbuli amesema:” Tuliwaruhusu wachezaji wetu walioitwa timu zao za taifa kwenda kama Burkina Faso, (Yacouba Songne) na DRC, (Congo) (Mukoko Tonombe) pia Jumamosi wachezaji walioitwa timu ya taifa walikwenda kambini.
“Wale wachezaji ambao walibakia walipewa mapumziko ya siku mbili yaani Jumamosi na Jumapili baada ya hapo wanarejea kambini.
“Leo, (Jumatatu) kikosi kinarejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zilizobaki za ligi pamoja na mechi za Kombe la Shirikisho,” amesema Bumbuli.
Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29 katika Kombe la Shirikisho ipo hatua ya nusu fainali na itacheza na Biashara United ya Mara.