news

BEKI ALIYEKUWA ANAWINDWA NA YANGA AMALIZANA NA SIMBA

admin June 9, 2021 4:47 pm


IMEELEZWA kuwa nyoa wa kikosi cha Ruvu Shooting, Edward Manyama amemalizana na mabosi wa Simba kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.


Nyota huyo ambaye amecheza Ruvu Shooting,  Namungo kwa sasa yupo ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen.

Habari zinaeleza kuwa ushindani mkubwa wa kusaka saini ya beki huyo ilikuwa kati ya Yanga na Simba ambao wote ni vigogo wa Kariakoo.

Yanga walianza kumfuatilia nyota huyo msimu uliopita alipokuwa ndani ya Namungo dili lake likabuma akaibukia ndani ya Ruvu Shooting.
Alipotafutwa Manyama azungumzie suala hilo alisema kuwa hajui jambo lolote.
ORODHA YA WALIOCHUKUA FOMU KUGOMBEA UONGOZI TFF VIDEO: OSCAR OSCAR ACHUKUA FOMU, TAZAMA MSAFARA WAKE ULIVYOKUWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply