Simba SC

SELEMAN MATOLA: KAZI BADO INAENDELEA

admin June 9, 2021 10:47 am


 KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya ili kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa kazi bado inaendelea.

 

 Mchezo wao wa mwisho kabla ya ligi kusimama kwa ajili ya kambi ya timu ya taifa ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Ruvu Shooting 0-3 Simba.

 

Matola amesema kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya kufikia malengo ambayo wamejiwekea kwa kuwa ushindani ni mkubwa.

“Kazi bado inaendelea kwani ligi haijaisha na tuna mechi mkononi ambazo tunapaswa kucheza jambo la msingi ni kuona kwamba mechi zetu ambazo zimebaki tunapata matokeo chanya ili tuweze kufikia malengo yetu.


“Wachezaji wanajuhudi na wanapaswa pongezi kwa kuwa wanatimiza majukumu yao hivyo kazi bado inaendelea kwa mechi zetu zijazo imani ni kwamba tutafanya vizuri,” amesema.

 

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya kwanza ina pointi 67 baada ya kucheza mechi 27.

VIDEO; OSCAR OSCAR ABAINISHA MALENGO YAKE ATAKAPOWANIA URAIS, AITAJA FIFA GOMES AAGIZA ‘BEKI LA DUNIA’ KUSAJILIWA SIMBA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply