UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hali ya kiungo wao Tonombe Mukoko, ambaye alipata majeruhi akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa kwa sasa inaendelea vizuri.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa walipata taarifa kuhusu kuumia kwa mchezaji wao.
Bumbuli amesema:-βTulikuwa na wasiwasi juu ya hali ya mchezaji Mukoko Tonombe ambaye aliumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Tunisia.
βIla kwa sasa tumepata taarifa kwamba anaendelea vizuri na tumewasiliana naye kama klabu na hatua inyofuata ni madaktari kuzungumza na madaktari wa huko ili kujua kwamba kama anaweza kukaa nje kwa muda gani,β amesema Bumbuli.