NYOTA wa Simba, Ibrahim Ajibu anatajwa kuwa yupo kwenye hesabu za Yanga ambapo tetesi zinaeleza kuwa amemalizana na mabosi wake hao wa zamani, meneja wake amesema kuwa bado kwa sasa Ajibu anafurahi kuwa ndani ya Simba ila lolote linaweza kutokea. Ameongeza pia kuna ofa kutoka timu ya Afrika Kusini pamoja na timu kubwa ndani ya ardhi ya Tanzania.