Simba SC

MZAWA JOHN BOCCO KUWEKA REKODI YA MABAO

admin June 12, 2021 4:47 pm


MSHAMBULIAJI na nahodha wa Simba, John 
Bocco, amebakisha mabao manne tu, ili kuandika historia mpya ya mabao ya kufunga ndani ya msimu mmoja akiwa na kikosi hicho.

Tangu ametua Simba, idadi kubwa ya mabao ambayo Bocco amewahi kufunga ndani ya msimu mmoja ni 16 aliyoyafunga msimu wa 2018/19, kabla ya hapo, Bocco msimu wa 2017/18 alifunga mabao 14 na msimu uliopita alifunga mabao 9 kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.

 Msimu huu tayari ana mabao 13.Mpaka sasa mshambuliaji huyo, ndiye kinara wa mabao ndani ya Simba kwa mabao yake hayo 13, amezidiwa bao moja pekee na kinara Prince Dube kutoka Azam.

 Kuhusu mipango yake Bocco amesema:- “Kama mshambuliaji nina kazi kubwa ya kuhakikisha ninaisaidia timu yangu kufikia malengo tuliyonayo msimu huu.

“Lakini nafurahia kasi niliyonayo, na nimejipanga kutumia kila nafasi nitakayoipata kufunga mabao mengi zaidi.”


VIDEO: OSCAR OSCAR AREJESHA FOMU, ATAJA CHANGAMOTO AMBAYO ALIYOKUTANA NAYO INJINIA YUPO KAZINI, UJANJA WA KAGERE WAANIKWA, NDANI YA SPOTI XTRA JUMAPILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply