Yanga SC

YANGA YATUMA SALAMU BIASHARA UNITED

admin June 14, 2021 10:47 am


 NYOTA wa kikosi cha Yanga, Saido Ntibanzokiza amesema kuwa wana imani watafanya vizuri kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa kati ya Juni 28 ambapo mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba na Azam FC.

Raia huyo wa Burundi amesema:”Tunajua kwamba Biashara United ni timu imara na inafanya vizuri lakini hatutaweza kuwaacha waweze kushinda kirahisi kwani nasi tunahitaji ushindi.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwa kupambana kwa mechi ambazo zimebaki kikubwa mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwa bao la Yacouba Songne ambaye alitumia pasi ya Saido.

ISHU YA YANGA KUMSAJILI KAMBOLE, KAIZER CHIEFS WATOA NENO YANGA YAPIGA HESABU YA POINTI 15 BONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply