Yanga SC

ISHU YA YANGA KUMSAJILI KAMBOLE, KAIZER CHIEFS WATOA NENO

admin June 14, 2021 9:47 am


 WAKATI Yanga ikiwa kwenye harakati za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji matata wa Kaizer Chiefs, Mzambia, Lazarous Kambole, uongozi wa Kaizer Chiefs umetoa neno juu ya dili hilo.

 

Ipo hivi; Inafahamika kuwa, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said yupo Afrika Kusini kwa ajili ya kufanikisha dili hilo, baada kumalizana na beki wa AS Vita, Djuma Shabani kwa mkataba wa miaka miwili.

 

Spoti Xtra linafahamu kila kitu juu ya dili la mshambuliaji huyo ambapo Kaizer wapo tayari kumuachia kutokana na kushindwa kuonesha ubora wake tangu alivyojiunga na timu hiyo mwaka 2019 akitokea Zesco United ya Zambia.

 

Kambole ameliambiaSpoti Xtra kuwa: “Sina sababu ya kudanganya juu ya hilo, lakini ukweli sijui kitu chochote kinachoendelea.

 

”Alipotafutwa meneja wa mawasiliano wa timu hiyo, Alpheus Maphosa ‘Vina’ juu ya kuzungumzia hilo, kwanza alionesha ukali akisema: “Siwezi kukubali kuongea na mwandishi iwe kwenye ukweli au uongo, naomba unithibitishie hizo taarifa za tetesi umezitolewa wapi.”

 

Baada ya kuthibitishiwa taarifa hizo juu ya Yanga kumtaka Kambole, akaibuka na kusema: “Unajua viongozi wa Kaizer wapo bize na mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa kama dili la mchezaji likiwa limekamilika nitakueleza mapema.”

VIDEO: KUNA WACHEZAJI WANAJUA GOLI KULIKO MBWANA SAMATTA YANGA YATUMA SALAMU BIASHARA UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply