kimataifa

ARGENTINA YATOSHANA NGUVU NA CHILE COPA AMERICA, MESSI ATUPIA KWA PIGO HURU

admin June 15, 2021 6:47 am


KWENYE mchezo wa Copa America uliochezwa usiku wa kuamkia leo Juni 15, timu ya taifa ya Argentina imetoshana nguvu na Chile kwa kufungana bao 1-1.

Lionel Messi alipachika bao bora kwa pigo huru dakika ya 33 liliwekwa usawa na Eduardo Vargas dakika ya 57.

Licha ya Messi kupachika bao hilo bora akiwa umbali wa yard 25 waliweza kuacha pointi mbili katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa uliochezwa Uwanja wa Olympic.

Kwenye mchezo huo Argertina walipiga jumla ya mashuti 18 na matano yalilenga lango huku Chile wakifanya hivyo mara 5, katika mashuti hayo ni manne yalilenga lango.

Kwenye msimamo wa kundi B, Paraguay inaongoza kundi ikiwa na pointi tatu huku Argertina na Chile zikiwa na pointi moja na Uruguay haina pointi sawa na Bolivia.

VIDEO: MASAU BWIRE AWEKA WAZI HESABU ZAO KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA SIMBA KAMILI KUIVAA POLISI TANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply