epl

KEPA WA CHELSEA KUIBUKIA LAZIO KWA MKOPO

admin June 16, 2021 2:47 pm


 KOCHA Mkuu wa Lazio, Maurizio Sarri amesema kuwa anahitaji saini ya kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Sarri anataka kuongeza nguvu katika kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Anataka kumpata mchezaji huyo kwa mkopo kipa huyo namba mbili wa Chelsea ili kumpa changamoto kipa namba moja wa Lazio ambaye alicheza ndani ya Liverpool, Pepe Reina.

Kepa alijiunga na Chelsea mwaka 2018 kwa dili la pauni milioni 17 amekuwa chaguo namba mbili huku namba moja akiwa ni Edouard Mendy ambaye amejiunga darajani msimu huu.

TANZIA: MZEE MATATA WA MIZENGWE AFARIKI DUNIA RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND YAWEKWA WAZI, CITY KUANZIA UGENINI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply