Home Burudani TANZIA: MZEE MATATA WA MIZENGWE AFARIKI DUNIA

TANZIA: MZEE MATATA WA MIZENGWE AFARIKI DUNIA

 


Muigizaji wa vichekesho wa kundi la Mizengwe, Jumanne Alela maarufu kwa jina la Mzee Matata amefariki dunia.

Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa jana Jumatano Juni 15, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha.

Aligaesha amesema msanii huyo amefariki dunia juzi saa tano na nusu usiku wa kuamkia jana.

“Msanii Bw. Jumanne Alela amefariki dunia juzi saa tano na nusu usiku wa kuamkia jana. Alilazwa tarehe 13.6. 2021” amesema Aligaesha

Enzi za uhai wake Mzee Matata alitamba na maigizo katika kikundi cha Mizengwe kilichokuwa na wasanii, Mkwere Original, Safina, Sumaku na Maringo Saba.

SOMA NA HII  KUTOKA KWENYE SIMULIZI ZA KNUD, MPAKA KWENYE USHINDI MKUBWA MERIDIANBET.....!