CRISTIANO Ronaldo nyota wa timu ya Taifa ya Ureno amevunja rekodi ya Michel Platini wa Ufaransa ya kufunga mabao mengi ndani ya UEFA European Championship.
Ushindi walioupata usiku wa kuamkia leo baada ya ubao wa Uwanja wa Ferenc Puskas kusoma Hungray 0-3 Ureno kumemfanya Ronaldo kuwa mfungaji bora wa muda wote katika UEFA European Championship.
Ni Raphael Guerreiro alianza kupachika bao la kwanza katika mchezo huo wa Euro 2020 kisha Ronaldo alipachika bao la pili dakika ya 87 kwa penalti na la tatu alipachika dakika ya 90+2
Mabao hayo mawili yanamfanya Robaldo kufikisha jumla ya mabao 11 katika Euro akiwa amecheza jumla ya mechi 22 huku Platini wa Ufaransa rekodi yake ilikuwa ni mabao 9 katika mechi tano ambazo alicheza ma nafasi ya tatu ni ya Alan Shearer wa England ambaye alitupia mabao 7 katika mechi 9 alizocheza.
Tofauti ya Mreno na Mfaransa huyo ni kwamba Platini alipachika mabao yote hayo katika mashindano ya mwaka 1984 huku Ronaldo akifunga mabao hayo katika mashindano matano tofauti.