Yanga SC

KUMBE! FARID MUSSA ALIUGUA GHAFLA KWA MKAPA, YACOUBA AREJEA

admin June 19, 2021 12:47 pm


HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa nyota wao wawili ambao ni Farid Mussa na Mukoko Tonombe wanaendelea vizuri.

Bumbuli amesema:”Hali za wachezaji kwa sasa ni nzuri tunamshukuru Mungu kwamba wachezaji wanaendelea vizuri.

“Farid Mussa aliugua ghafla muda wa mapumziko hivyo alibadilishwa kutokana na kupata allergy (mzio) na madaktari wamesema kuwa anaendelea vizuri.

“Mukoko Tonombe anaendelea vizuri madaktrai wameshauri kwamba apewe muda wa uangalizi kwa kuwa huenda likawa ni lile tatizo ambalo alipata akiwa na timu ya taifa ya Congo.

Wachezaji hawa walipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Uwanja wa Mkapa ambapo ubao ulisoma Ruvu Shooting 2-3 Yanga.

Kuhusu Yacouba Bumbuli amesema:-“Yacouba Songne amerejea na yupo kambini akiwa na wachezaji wakiwa kwenye maandalizi ya mechi yetu ijayo dhidi ya Mwadui FC,” amesema.

Yanga kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya pili imekusanya jumla ya pointi 64 baada ya kucheza jumla ya mechi 30 inakutana na Mwadui FC iliyo nafasi ya 18 na pointi 19.

POLISI TANZANIA YAZITAKA POINTI TATU ZA SIMBA LEO KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA POLISI TANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply