Ligi Kuu

POLISI TANZANIA YAZITAKA POINTI TATU ZA SIMBA LEO

admin June 19, 2021 12:47 pm


GEORGE Mketo, Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania amesema kuwa wapo tayari kuwakabili wapinzani wao Simba.

Polisi Tanzania itaingia Uwanja wa CCM Kirumba leo saa 10:00 kusaka pointi tatu mbele ya  Simba.

Katika mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Simba 2-0 Polisi Tanzania hivyo leo utakuwa ni mchezo wa kisasi.

Msimamo unaonyesha kwamba Polisi Tanzania ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 41 na Simba ipo nafasi ya kwanza na pointi 67.

Mketo amesema:”Tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu.

“Wachezaji wanajua kwamba Simba ni timu kubwa na tunawaheshimu lakini tunahitaji pointi tatu muhimu,” amesema.


VIDEO: MASHABIKI WA YANGA WAMUOMBEA MSAMAHA METACHA KUMBE! FARID MUSSA ALIUGUA GHAFLA KWA MKAPA, YACOUBA AREJEA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply