Simba SC

MABAO 20 YAREJEA RASMI SIMBA

admin June 21, 2021 4:47 pm


CLATOUS Chama, mtambo wa mabao ndani ya Simba amerejea ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na matatizo ya kifamilia.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Chama raia wa Zambia amehusika katika jumla ya mabao 20 kati ya 65 ambayo yamefungwa ndani ya mechi 28.

Chama alikuwa nchini Zambia baada  ya mkewe Mercy Mukuka kutangulia mbele za haki, Mei 29 hivyo hakuwepo katika mechi zilizofuata ndani ya Simba.

Alikosekana katika mchezo dhidi ya Namungo 1-3 Simba, Mei 29, Ruvu Shooting 0-3 Simba, Juni 3 na Polisi Tanzania 0-1 Simba, Juni 19.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Simba waeandika kwamba Amerudi, triple C.


MSHAMBULIAJI YANGA KUFUNGASHIWA MABEGI MAZIMA KIUNGO KUTOKA NIGERIA AKUBALI KUTUA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply