kimataifa

SANCHO APIGIWA HESABU NA MANCHESTER UNITED, CHELSEA

admin June 22, 2021 9:47 am


 MANCHESTER United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solksjaer bado wanaipigia hesabu saini ya winga wa Borussia Dortmund na nyota wa timu ya taifa ya England, Jadon Sancho. 

United imekuwa ikipambana kupata saini ya nyota huyo kwa muda mrefu jambo ambalo limekwama kukamilika.

Kwa sasa nyota huyo anatajwa kuwa kwenye hesabu za Chelsea pia ambao nao wanahitaji kupata saini yake pamoja na Manchester City ambazo zipo mstari wa mbele kupata saini ya nyota huyo mwenye miaka 21.

Ripoti zimeeleza kuwa mabosi wa Manchester United jicho lao la kwanza kwenye dirisha la usajili ni kwa Sancho na wanahitaji kumuona akiwa katika Uwanja wa Old Trafford msimu ujao.

Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Dortmund, Hans Joachim  aliweka wazi kuwa klabu hiyo inajiandaa kumuuza Sancho kwa ofa nzuri ambayo itafika mezani.



VIDEO:CHAMA AREJEA SIMBA, WAZEE WA YANGA WAUNGA MKONO MABADILIKO KIPA METACHA MNATA ALICHEZA YANGA BILA KULIPWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply