Home Tetesi za usajili NYOTA HAWA 7 WATAJWA KUINGIA ANGA ZA YANGA ILI WAMWAGE SAINI

NYOTA HAWA 7 WATAJWA KUINGIA ANGA ZA YANGA ILI WAMWAGE SAINI


 IMEELEZWA kuwa kwa sasa Klabu ya Yanga ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi hicho huku nyota 7 wakitajwa kuingia kwenye rada zao.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi kwa sasa ipo Tabora kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa kesho Juni 25.

Wachezaji ambao wanatajwa kuwa kwenye mazungumzo na Yanga ni pamoja na Lazaros Kambole, Anthony Akumu (Kaizer Chiefs), Mercey Ngimbi (Miniema FC), Ben Malango (Raja Casablanca) Ferjan Sassi (Zamalek), Cleophance Mkandala wa Dodoma Jiji na kipa wa Tanzania Prisons Jeremia Kisubi.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa muda wa usajili bado ila watafanya kwa umakini usajili kwa kutegemea ripoti ya kocha.

SOMA NA HII  MANARA AITOA YANGA KWENYE MBIO ZA UBINGWA...AWAPA 'MAKAVU LIVE' MASHABIKI WAO...