Yanga SC

JK AFUNGUKA MAHABA YAKE KWA YANGA..AWAPA KAZI YA KUFANYA DHIDI YA SIMBA

admin June 28, 2021 9:22 am


ALIYEKUWA Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema matumaini yake anaona kabisa timu yao ya Yanga inashinda katika mchezo wao wa Jumamosi.

Yanga Jumamosi inakuwa na kibarua kigumu dhidi ya watani wao Simba mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni.

Awali mchezo huo ulitakiwa kuchezwa Mei 8 lakini mchezo huo ulisogezwa mbele baada ya kutokea mtafaruku wa kubadilishwa muda kutoka saa 11 jioni na kupelekwa saa 1 usiku.

Kikwete amesema yeye ni Yanga na amekuwa na timu hiyo kwa nyakati zote.

“Yanga ikifanya vizuri ninafurahia, Yanga ikifanya vibaya ninasononeka kweli,” alisema Kikwete.

BURNA BOY ASHINDA TUZO YA BET KIKWETE ASIMULIA JINSI ALIVYOSHIRIKI ‘KULOGA’ ILIA YANGA ISHINDE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply