Home Simba SC ALICHOSEMA MAMA AKE MKUDE..BAADA YA MWANAE KUPIMWA AKILI

ALICHOSEMA MAMA AKE MKUDE..BAADA YA MWANAE KUPIMWA AKILI


MAMA mzazi wa kiungo wa Simba, Jonas Mkude, Grace Shimba amezungumzia msala alionao mwanae hasa ishu ya kutakiwa kwenda kupimwa.

Mkude yupo matatani na mabosi wake wa Simba kwa kosa la utovu wa nidhamu na alipelekwa kwenye Kamati ya Maadili, chini ya Mwenyekiti wake, Suleiman Kova ilishindwa kutoa hukumu ikitakiwa apelekewa hospitali kupimwa na kuzua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, mama huyo alisema; “Imeniumiza sana kwani nimemzaa Jonas akiwa na akili timamu na nimeyaona yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii yananipa mawazo ila sina chakufanya. “Utumbo unanikata kwani nimembeba miezi tisa tumboni kwangu, ilinishtua sana kuambiwa anatakiwa kwenda kupima wengine wakidai akili, ila namuombea kwa Mungu amlinde.”

Alisema alimuita na kumkalisha chini kumpa moyo . “Nilimzaa akiwa mzima, pia anapaswa kumuomba Mungu amsimamie, ujue siwezi kuingilia mambo ya ajira yake ila imenigusa kuhusu akili yake,” alisema Grace.

Mbali na hilo, alimtaka kijana wake kuwa mtulivu kwenye kipindi cha mpito kwake na kwamba hawezi kushindana na kila kitu kinaongelewa mitandaoni.

“Asubiri maamuzi na klabu, ndio maana nimesema hilo siwezi kuliingilia, pia anapaswa kunyamaza kimya na sio kujibizana na kila mtu,” alisema.

Mkude alinza kucheza kikosi cha kwanza cha Simba msimu wa 2011.

SOMA NA HII  MANGUNGU ATOA KAULI YA KIBABE LEO SIMBA DHIDI YA POWER DYNAMO