Home Simba SC GADIEL MICHAEL AONDOLEWA KWENYE MIPANGO YA SIMBA, HATIHATI KUACHWA MAZIMA

GADIEL MICHAEL AONDOLEWA KWENYE MIPANGO YA SIMBA, HATIHATI KUACHWA MAZIMA


GADIEL Michael nyota wa kikosi cha Simba inaelezwa kuwa jina lake limewekwa kando kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.

Nyota huyo ambaye ni beki wa kushoto aliibuka ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes akitokea Klabu ya Yanga.

Habari zinaeleza kuwa kushindwa kufiti kikosi cha kwanza ni sababu inayofanya nyota huyo kupigiwa hesabu za kuachwa.

Uwepo wa beki ambaye ni nahodha, Mohamed Hussein, ‘Tshabalala’ kuwa katika ubora ni sababu inayofanya uongozi wa Simba kufikiria kumuacha.

Kuhusu suala la usajili, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah, ‘Try Again’ amesema kuwa muda wa usajili bado na mipango yote ipo kwa kocha.

SOMA NA HII  LIGI YA MABINGWA AFRIKA:AS VITA 0-1 SIMBA