Home CAF KAIZER CHIEFS YAWAPA TABU WAYDAD LIGI YA MABINGWA AFRIKA

KAIZER CHIEFS YAWAPA TABU WAYDAD LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 SAMIR Nurkovic nyota wa kikosi cha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mohammed V, Wydad waliutawala mchezo kwa asilimia 79 huku Kaizer Chiefs ambao walikuwa ugenini walikuwa na asilimia 21.

Ilikuwa dakika ya 34, Samir alipachika bao hilo na kufanya timu yao ipige jumla ya mashuti matatu huku lililolenga lango likiwa moja lililojaa wavuni.

Wydad wao walipiga jumla ya mashuti 28 na ni 8 yalilenga lango na katika pasi Wydad walipiga jumla 670 huku Kaizer Chiefs ambao walizima ndoto za Simba kutinga hatua ya nusu fainali walipiga pasi 183.

Mtanzania Simon Msuva alianzia benchi na hata alipoingia ngoma ilikuwa nzito.

SOMA NA HII  BAADA YA KUICHAPA YANGA , RIVER PLATE WAFUNGUKA HUJUMA ZA YANGA..WAITAJA ENYIMBA FC