ALIYEKUWA Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewasili katika mkutano mkuu wa Yanga saa 11:59 akiwa ndiye mgeni rasmi wa mkutano huo.
Kabla ya Kikwete hajaingia viongozi wa Yanga walitoka nje na kupanga mstari kwa ajili ya kusalimiana naye na kupata picha ya pamoja.
Mstari huo uliongozwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk Mshindo Msolla na Kikwete aliposhuka tu alianza kusalimiana na viongozi hao huku akiongozana na Msolla.
Maofisa usalama walihakikisha eneo lote liko salama kwani kabla hajafika walikuwa wametanda kuweka eneo likiwa lipo salama.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Kikwete kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli za klabu hiyo baada ya awali kuwa katika ugeni rasmi kwenye Kubwa Kuliko.