Home Azam FC MORRIS: BADO TUNA KAZI KUBWA YA KUFANYA

MORRIS: BADO TUNA KAZI KUBWA YA KUFANYA


 AGREY Moriss, nahodha wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa wanaamini kwamba watapambana kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zilizobaki ili kufikia malengo ambayo walianza nayo mwanzo wa msimu.

Mzawa huyo ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, George Lwandamina alikuwa amevaa kitambaa chake wakati timu hiyo ikitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rhino Rangers.

Hatua ya nusu fainali itacheza na Simba ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ambaye aliongoza kikosi chake kushinda mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji.

Morris pia amekuwa na zali la kufunga mabao muhimu ambapo alipachika bao la ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC wakati ubao wa Azam Complex uliposoma Azam FC 2-1 KMC.

Nyota huyo amesema;”Bado tuna kazi kubwa ya kufanya kufikia malengo yetu imani yetu ni kwamba bado tuna kazi ya kufanya na kwa namna hali ilivyo tupo kwenye mwendo mzuri.

“Kilichobaki ni kila mmoja kuweza kushinda mechi zake ambazo atacheza hicho ndicho ambacho tunakifanya, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  AZAM FC :MECHI ZA YANGA NA SIMBA NI PRESHA,ILA HATUNA HOFU