Home Simba SC MUGALU : NIPO FITI KABISA …YANGA WAJIPANGE

MUGALU : NIPO FITI KABISA …YANGA WAJIPANGE


STRAIKA wa Simba, Chriss Mugalu alishindwa kucheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Azam baada ya kupata maumivu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania, lakini fasta taarifa zikufikie kuwa jamaa kaiwahi Kariakoo Derby ya Julai 3.

Mugalu alipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania uliopigwa jijini Mwanza baada ya kupigwa kiatu na beki Kelvin Yondani na kumfanya atolewe nje na kulikosa pambano lililopita la Ligi dhidi ya Mbeya City na ule wa ASFC, lakini kwa sasa anaendelea vyema na imani yake anaweza kuliamsha kwenye Kariakoo Derby wiki ijayo, jijini Dar es Salaam.

Straika huyo kutoka DR Congo alisema alitamani kucheza mechi hiyo ili kuisaidia timu yake kupata ushindi lakini maumivu yalimfanya ashindwe kuendelea lakini hata baadae alipokuja kupata tiba zaidi alitakiwa kupata na muda wa kupumzika.

“Nilipata tiba nzuri kutoka kwa madaktari na yalikuwa maumivu pamoja na mshtuko baada ya kuchezewa rafu ya nguvu na Yondani lakini kwa sasa maendeleo yangu ni mzuri tofauti na awali,” alisema Mugalu na kuongezea;

“Hali ambayo nilikuwa nayo mwanzo ni tofauti na sasa kwani naendelea vizuri baada ya kupata matibabu na programu maalumu ya mazoezi ya gym ambayo nilipewa nimeimaliza kwa kufanya kama ilivyopaswa. Ambacho nasubiria hapa ni kuungana na wachezaji wenzangu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo unaofuata lakini kimaendeleo sasa nipo fiti.”

Hata hivyo licha ya kiu yake ya kulicgheza pambano dhidi ya Yanga ambalo awali lilikwama kupigwa Mei 8, bado maamuzi yatabaki kwa Kocha Didier Gomes, kwani bado ana mashine za maana katika safu ya usahmbuliaji akiwamo John Bocco, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu na Miraji Athuman.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WASAUZI...GOMES AIBUKA UPYA SIMBA....AFUNGUKA HAYA KUHUSIANA NA WACHEZAJI...