Home Ligi Kuu POLISI TANZANIA YAIPIGIA HESABU SIMBA

POLISI TANZANIA YAIPIGIA HESABU SIMBA

TIMU ya Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini imeanza hesabu za kuivutia kasi Simba kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 19, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa timu hizo kukutana kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 2-0.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa malengo ya Polisi Tanzania ni kulipa kisasi cha kufungwa na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes huku wao Polisi Tanzania wakipiga hesabu za kulipa kisasi.
Akizungumza na Saleh Jembe, kiungo wa Polisi Tanzania, Hassan Nassoro amesema kuwa tayari wameanza mazoezi kwa ajili ya mechi zao zilizobaki ikiwa ni pamoja na ule dhidi ya Simba.
“Mchezo wetu ujao wa kwenye ligi ni dhidi ya Simba hivyo tunaamini kwamba tutapambana kupata ushindi kwa kuwa inawezekana na kwenye mpira kila kitu kinatokea.
“Muda wa mapumziko kwetu umeisha na sasa tupo kazini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zetu zijazo hivyo tunaamini kwamba tutafanya vizuri na kupata pointi tatu kwenye mechi zetu zijazo,” alisema nyota huyo.
Kwenye msimamo, Polisi Tanzania ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 41 inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 67.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA TANZANIA PRISONS DHIDI YA SIMBA, UWANJA WA MKAPA