Home epl SANCHES AINGIA ANGA ZA ARSENAL

SANCHES AINGIA ANGA ZA ARSENAL


KIUNGO wa timu ya taifa ya Ureno anayekipiga ndani ya Klabu ya Lille inayoshiriki Ligue 1, Renato Sanches amewekwa kwenye rada za Arsenal na Liverpool za England. 

Nyota huyo mwenye miaka 23, leo Juni 27 anatarajiwa kuwa katika kikosi kitakachopambana na Ubelgiji katika hatua ya 16 bora Euro 2020.

Ripoti zinaeleza kwamba, Kocha Mkuu wa Arsenal,  Mikel Arteta anamfuatilia kwa ukaribu nyota huyo ili ajiunge nao msimu ujao katika eneo la kiungo.

Kwenye Euro 2020 alianza mchezo mmoja kikosi cha kwanza huku michezo miwili akitokea benchi na aliweza kuonyesha kiwango bora kwa timu hiyo jambo ambalo limezivutia timu nyingi.


SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO WA DODOMA JIJI WAWEKWA RADA NA YANGA