Home Yanga SC YANGA KUSAJILI MAJEMBE MAPYA NAFASI YA USHAMBULIAJI, BEKI

YANGA KUSAJILI MAJEMBE MAPYA NAFASI YA USHAMBULIAJI, BEKI


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba utafanya usajili katika eneo la ushambuliaji ili kuongeza nguvu kwa ajili ya msimu ujao.


Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 na safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 49 ikiwa imecheza jumla ya mechi 31.

Pia safu ya ulinzi inayoongozwa na Bakari Mwamnyeto imeruhusu jumla ya mabao 21 huku ile ya Simba inayoongozwa na Joash Onyango ikiwa imeruhusu mabao 11 kati ya mechi 27.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wameona mahali ambapo kuna mapungufu hivyo watafanyia kazi kwa kusajili kwenye nafasi ya ushambuliaji na ulinzi.

“Msimu huu kuna mambo tumeyaona na kilichobaki kwa sasa ni wazi kwamba bado tunajenga timu, tutaongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji na ulinzi ili tuweze kufanya vizuri msimu ujao.

“Mashabiki waendelee kutupa sapoti wasikate tamaa tupo imara na tutafanya vizuri bila mashaka kwani kujenga timu kunahitaji muda,” amesema Nugaz.

  Miongoni mwa wachezaji ambao walisajiliwa na Yanga ni pamoja na Wazir Junior mwenye mabao mawili, Michael Sarpong mwenye mabao manne, Fiston Abdulazack mwenye bao moja ndani ya ligi.

 

SOMA NA HII  VIGOGO WA SOKA AFRIKA...WAIOGOPA MECHI SIMBA NA YANGA...WAPATA VIGUGUMIZI