Home Yanga SC YANGA: MANJI HAKUFUKUZWA, RUKSA KUWEKEZA

YANGA: MANJI HAKUFUKUZWA, RUKSA KUWEKEZA


 UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeweka wazi kwamba aliyekuwa mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuf Manji ana nafasi ya kurudi ndani ya timu hiyo kwa kuwa hakufukuzwa.

Taarifa zinaeleza kuwa Manji yupo Bongo na hesabu zake kubwa pia ni kurejea katika uwekezaji ndani ya kikosi cha Yanga.

Juni 27, Yanga wanakwenda kwenye mkutano wa mkuu huku moja ya ajenda ikiwa ni mabadiliko na inatajwa kuwa huenda tajiri huyo akaibukia ndani ya mkutano huo.

Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema kuwa Manji hakufukuzwa ndani ya Yanga na akihitaji kurudi atapewa fursa.

“Jambo la muhimu ni kukidhi vigezo na habari njema ni kwamba mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu unaruhusu wawekezaji, aje tutampokea na si yeye tu, tunaruhusu wawekezaji wengine,” .

SOMA NA HII  SIMBA, YANGA WAWEKA WAZI MALENGO YA USAJILI WAO DIRISHA KUBWA LA USAJILI