Home Azam FC YANGA YAINGIA ANGA ZA AZAM FC KUMTAKA SURE BOY

YANGA YAINGIA ANGA ZA AZAM FC KUMTAKA SURE BOY

[the_ad id="25893"]


KIUNGO wa Azam FC,  Salum Aboubakary, ‘Sure Boy’ anatajwa kuwa katika rada za mabosi wa Yanga huku wenye mali nao wakihitaji huduma yake.

Ikumbukwe kuwa msimu uliopita wa 2019/20, Yanga walikuwa na mpango wa kumsajili nyota huyo ambapo ishu ilikuwa katika dau.

Yanga wao waliweka dau la milioni 40 jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Azam FC wawaambie kwamba waongeze dau kwa kuwa Sure Boy ni nembo ya Azam FC jambo lililokwamisha dili hilo.

Kwa sasa mkataba wa nyota huyo ambaye yupo katika kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars unakaribia kumeguka jambo ambalo linawapa nguvu Yanga kuipata saini yake.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria alisema kuwa ni ngumu kwa timu hapa Bongo kumchukua mchezaji ambaye anahitajika na Azam FC.

“Kwetu sisi Azam FC kumuacha mchezaji tunayemtaka labda tuamue sisi ila hakuna ambaye anaweza kushindana nasi, kama biashara sisi tunafanya mpaka tuamue wenyewe,” .


SOMA NA HII  WAKATI LEO NDIO SIKU YA MWISHO USAJILI BONGO....AZAM KUTETEMESHA JIJI.. FEI TOTO ATAJWA..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here